Nina ujauzito. Ninawezaje kutumia Clue sasa?

Ukipata ujauzito ukiwa katika hali ya Clue-Ufuatiliaji wa hedhi, unaweza kubadilisha hadi hali ya Clue Ujauzito wakati wowote. Kila mtu anayetumia Clue anaweza kuona taarifa za kila wiki za Clue Ujauzito kuhusu ukuaji wa fetasi kwenye skrini ya mwanzo, ili uweze kufuatilia jinsi ujauzito wako unavyoendelea.

 

Ikiwa una Clue Plus, unaweza pia kutumia vipengele vya kulipia vya Clue Ujauzito vinavyokupa usaidizi zaidi katika kila miezi mitatu ya ujauzito. Hivi ni pamoja na vipengele vya kufuatilia vinavyohusu ujauzito, taarifa za kila wiki kuhusu kinachoendelea katika mwili wako na kwa fetasi, pamoja na taarifa za kina zaidi na makala zilizoandikwa na wataalamu wetu. 

 

Ili kubadilisha hali, fuata hatua hizi: Gusa Menyu zaidi (= iliyo juu kulia) katika programu ya Clue > Chagua “Hali” > Chagua Clue Ujauzito > Gusa “Badilisha hali”. 

 

Ukiendelea kutumia hali ya Clue-Ufuatiliaji wa hedhi wakati una ujauzito, ujauzito wako utaonekana kama “mzunguko” mmoja mrefu kwa sababu hutafuatilia hedhi mpya. Hedhi yako itakaporudi baada ya ujauzito, unaweza kuanza kuifuatilia tena. Ili kuhakikisha kuwa ujauzito hauathiri mahesabu ya mzunguko wako, unaweza kuficha “mzunguko” huo mrefu kwenye mahesabu ya Clue kwa kufuata maelekezo hapa. Hii inaweza kusaidia kuhakikisha kuwa makadirio ya Clue yanaendelea kuwa sahihi baada ya ujauzito. 

 

Jifunze zaidi kuhusu ujauzito, kujifungua na kipindi cha baada ya kujifungua katika makala hizi.

------

Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii: 
Instagram, TikTok na LinkedIn

Was this article helpful?
1 out of 1 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk