Muunganisho wa Clue na Apple Health unakuwezesha kusawazisha taarifa zako za hedhi za Clue na Apple Health. Hii inajumuisha siku unazofuatilia hedhi yako pamoja na mtiririko wa hedhi. Kumbuka kuwa Clue hukuruhusu kufuatilia mtiririko wa hedhi kama “Mzito” au “Nzito sana”, lakini Apple Health itachukulia zote mbili kama “Mzito”. Muunganisho huu haujumuishi kuleta taarifa ulizofuatilia hapo awali.
Ili kuleta taarifa zako za hedhi kwenye Apple Health, fuata hatua hizi:
- Fungua programu ya Clue.
- Nenda kwenye Menyu zaidi, kwa kugusa alama ya “=” iliyo upande wa juu kulia kwenye Mwonekano wa Mzunguko.
- Gusa 'Mipangilio’.
- Gusa “Apple Health”, kisha gusa “Nenda kwenye Mipangilio”.
- Katika Mipangilio ya kifaa chako, fungua “Health”.
- Gusa "Upatikanaji wa Data & Vifaa".
- Chini ya "Programu na huduma", gusa "Clue".
- Toa idhini ili Clue iweze kushiriki tarehe za mzunguko wako na Apple Health.
Kuanzia sasa, unapofuatilia hedhi yako katika Clue, taarifa zitasawazishwa na Apple Health. Kumbuka kuwa ni taarifa za hedhi unazofuatilia katika Clue baada ya kutoa ruhusa ya kusawazisha na Apple Health pekee ndizo zitakazohamishwa. Kama njia mbadala, unaweza kufuta taarifa za awali na kuziweka tena, kisha zinapaswa kusawazishwa.
Kwa sasa, haiwezekani kuleta taarifa kutoka Apple Health kwenda Clue.
------
Hujapata kile ulichokuwa ukitafuta? Kwa taarifa zaidi kuhusu mada hii, soma makala zifuatazo:
Ninawezaje kupata nakala ya taarifa zangu za Clue?
Ninawezaje kudhibiti taarifa zangu?
Ninaweza kushiriki maoni yangu wapi?
------
Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii:
Instagram, TikTok na LinkedIn