Makadirio na wastani wangu hukokotolewaje?

Clue hukokotoa makadirio na wastani wako kwa kuendelea kuchanganua taarifa unazofuatilia.

Makadirio na wastani mwingi hutegemea sehemu fulani tu ya taarifa zako ulizofuatilia hapo awali. Makadirio hutegemea taarifa za mizunguko yako 12 iliyopita, huku wastani ukitegemea taarifa za mizunguko yako 6 iliyopita. Hesabu hii hutumika kukokotoa urefu wa mzunguko, urefu wa hedhi, muda wa PMS na kutabiri wakati ambapo PMS inaweza kutokea.

Kutumia taarifa chache za hivi karibuni kwa njia hii husaidia algoriti ya Clue kuendana na mambo ya muda mfupi katika mazingira yanayokuathiri, pamoja na mabadiliko ya muda mrefu mwili wako unapopitia hatua mbalimbali za maisha.

Ovulesheni hukokotolewa kwa njia tofauti. Hukokotolewa kwa kuhesabu kurudi nyuma siku 13 kutoka siku ambayo hedhi yako inayofuata inakadiriwa kuanza. Kipimo chanya cha ovulesheni ulichofuatilia au taarifa za joto la msingi la mwili (BBT) zinaweza pia kuathiri hesabu za Clue.

 

------

Hujapata kile ulichokuwa ukitafuta? Angalia makala zifuatazo kwa maelezo zaidi kuhusu mada:

Je, ninahitaji kufuatilia kila siku?

------

Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii: 
Instagram, TikTok na LinkedIn

Was this article helpful?
0 out of 1 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk