Kwa nini Clue inaonyesha hedhi ndefu kuliko niliyofuatilia?

Huenda hedhi yako ya mwisho ilikuwa fupi kuliko urefu wako wa kawaida wa hedhi.

Clue hukokotoa wastani wa urefu wa hedhi yako kulingana na taarifa za mizunguko yako 6 iliyopita, kisha hutumia wastani huo kuonyesha makadirio ya hedhi kwa rangi ya waridi isiyokolea. Unaweza kuona wastani wa urefu wa hedhi yako katika kichupo cha Uchambuzi.

Kwa mfano, ikiwa umefuatilia siku 4 za hedhi, siku hizo zitaonekana kwa rangi nyekundu katika mwonekano wa mzunguko na mwonekano wa kalenda. Lakini ikiwa programu inajua kuwa wastani wa urefu wa hedhi yako ni siku 6, itaonyesha makadirio kwa rangi ya waridi isiyokolea katika siku ya 5 na ya 6.

------

Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii: 
Instagram, TikTok na LinkedIn

Was this article helpful?
0 out of 1 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk