Clue ina kanuni gani kuhusu ushirikiano na chapa nyingine?

Katika Clue, jamii yetu ndiyo kipaumbele chetu. Ndiyo maana mtindo wetu wa biashara unalenga kuongeza idadi ya usajili kwa kutengeneza vipengele vyenye manufaa makubwa ambavyo tunaamini vina thamani na vinawanufaisha watu wanaotumia Clue. Kwa kufanya hivyo, programu yetu inawahudumia tu watu ambao tumeitengenezea, si maslahi ya kampuni za bima, madalali wa data au mtu mwingine yeyote. 

Kwa sababu hii, kila ushirikiano tunaoufikiria au kuanzisha hupitiwa kwa makini sana kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:

  1. Je, unalinda maslahi na/au kuleta manufaa kwa jamii yetu?
  2. Je, unasaidia kuboresha, kuunga mkono au kuendeleza afya na ustawi wa wanawake na watu wenye mizunguko?
  3. Je, una msingi thabiti wa kisayansi na kimaadili?
  4. Je, unaendana na maono yetu ya kutokuwa na vizuizi, dhana potofu wala miiko? 
  5. Je, mshirika anafuata masharti madhubuti ya ulinzi wa data kulingana na GDPR ya Umoja wa Ulaya?

 

Daima tuko tayari kuzingatia ushirikiano na washirika ambao wanaweza kusaidia kuendeleza dhamira yetu, kunufaisha jamii yetu au kufanya Clue ipatikane kwa watu wengi zaidi duniani. Jambo ambalo hatutafanya kamwe, wala hatutawahi hata kulifikiria, ni kuuza data binafsi.

Was this article helpful?
0 out of 0 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk