Clue Plus inajumuisha nini?

Clue Plus hukupa ufikiaji wa vipengele, hali na manufaa mbalimbali vya premium vinavyotegemea ushahidi wa kisayansi. Fikiria kama mwenzi wako wa afya ambaye yuko pamoja nawe kila hatua. 

Ukiwa na Clue Plus unapata:

  • Makadirio ya kina ya mzunguko. Panga hadi miezi 12 mapema kwa kutumia makadirio ya hedhi, PMS na dirisha la uzazi katika mwonekano wa kalenda.

     
  • Makadirio ya maumivu ya tumbo wakati wa hedhi. Jua wakati ambapo huenda ukapata maumivu ya tumbo wakati wa hedhi, upate vidokezo vya kupunguza maumivu na ufahamu kuhusu historia yako ya kufuatilia maumivu hayo.
     
  • Ufikiaji kamili wa kichupo cha Yaliyomo. Soma vidokezo, ushauri na makala za elimu zilizoandikwa na timu ya Clue ya waandishi wa sayansi, wataalamu wa kliniki na wataalamu wa afya.
     
  • Vipengele vya ziada kwenye kichupo cha Uchambuzi. Elewa vizuri zaidi mifumo ya mzunguko wako kwa uchambuzi wa mtiririko wa hedhi na maumivu ya hedhi, chati za Joto la msingi la mwili za kufuatilia mabadiliko ya halijoto yako, na muhtasari kamili wa mzunguko unaoonyesha data zako zote za ufuatiliaji sehemu moja.
     
  • Vichujio vya kalenda. Chagua hadi dalili au mambo matatu uliyofuatilia ili kuchuja mwonekano wa kalenda na kuona kwa urahisi mienendo ya miezi iliyopita.
     
  • Clue Connect. Shiriki maelezo ya mzunguko wako na mwenzi, rafiki au mwanafamilia kwa kutumia kipengele chetu kilichoboreshwa cha Clue Connect.
     
  • Vipengele 10 vya Premium vya ufuatiliaji. Gundua miundo zaidi katika mzunguko wako kwa kutumia vipengele vya ziada vya ufuatiliaji kama vile “Ubora wa usingizi”, “Mkojo”, “Vulva na uke” na “Virutubisho”.
     
  • Lebo maalum zisizo na kikomo. Binafsisha jinsi unavyofuatilia kwa kutumia Lebo maalum zisizo na kikomo, ili uweze kufuatilia chochote kinachohusiana na mzunguko wako wa kipekee na ambacho ni muhimu kwako.
     
  • Huduma ya wateja ya hali ya juu. Pata usaidizi kutoka kwa timu yetu maalum ya Usaidizi wakati wowote unapouhitaji, iwe unataka kutupa maoni au kuuliza maswali.
     
  • Clue Kutafuta Ujauzito. Ongeza nafasi zako za kupata ujauzito kwa hali iliyoundwa kuwa mwongozo wako binafsi katika safari ya kutafuta ujauzito.
     
  • Vipengele vya Premium vya Clue Ujauzito. Fuatilia ukuaji wa kijusi na ujauzito wako kwa ufahamu na mwongozo wa kila wiki, ufuatiliaji mahususi kwa ujauzito na makala za kina.
     
  • Hali ya Clue kabla ya ukomo wa hedhi. Elewa vizuri zaidi mabadiliko yako kuelekea ukomo wa hedhi kwa kutumia hali yetu iliyoundwa kufuatilia mabadiliko yote unayopitia kabla ya ukomo wa hedhi.
     
  • Muunganisho wa Oura, Withings, Ultrahuman, Whoop, Polar, Huawei, Luna na Apple Watch (kwa vifaa vya iOS). Unganisha kifaa cha kuvaa unachopendelea ili kusawazisha taarifa zako za usingizi, joto na mapigo ya moyo na Clue.
     
  • Muunganisho wa Fitbit. Unganisha kifaa cha kuvaa unachopendelea ili kusawazisha taarifa zako za usingizi na mapigo ya moyo na Clue.
     
  • Maelezo ya kukusaidia katika ufuatiliaji wako. Gusa “Jifunze zaidi” kando ya kila kipengele cha ufuatiliaji ili ujue mambo ambayo kwa kawaida hutokea, kwa nini ni muhimu kuyafuatilia na wakati wa kutafuta ushauri wa matibabu. Unaweza pia kupata taarifa hizi zote kwenye Mwongozo wa ufuatiliaji, katika sehemu ya Rasilimali kwenye menyu kuu ya Mwonekano wa Mzunguko.


Uko tayari kujaribu Clue Plus? Fuata hatua hizi:

  1. Fungua programu ya Clue. 
  2. Nenda kwenye Menyu zaidi, kwa kugusa alama ya “=” iliyo upande wa juu kulia kwenye Mwonekano wa Mzunguko.
  3. Gusa bango la Clue Plus.
  4. Chagua mpango wako (wa kila mwezi au wa kila mwaka), kisha gusa “Jisajili”.
  5. Thibitisha usajili wako kupitia Apple App Store au Google Play Store.
  6. Umemaliza! Vipengele vyako vipya vya Clue Plus vitaonekana kiotomatiki kwenye programu.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu Clue Plus katika makala hii. 

------

Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii: 
Instagram, TikTok na LinkedIn

Was this article helpful?
0 out of 0 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk