Jinsi ya kufuatilia dalili na matukio yanayohusiana na mzunguko

 

Mbali na hedhi, kuna dalili na matukio mengine mengi yanayohusiana na mzunguko ambayo unaweza kufuatilia kwenye Clue. Baadhi yake ni PMS, maumivu, hisia, hamu ya kufanya ngono na ngozi. Ili kufuatilia dalili na matukio yanayohusiana na mzunguko wako, fuata hatua hizi:

 

  1. Fungua programu ya Clue.
  2. Gusa “Fuatilia”, au nenda kwenye Mwonekano wa Kalenda.
  3. Gusa tarehe unayotaka kufuatilia.
    • Kwenye Mwonekano wa Kalenda, utahitaji kugusa tarehe hiyo mara mbili.
  4. Telezesha chini na utafute kategoria unayotaka kufuatilia.
    • Kategoria za ufuatiliaji ni makundi kama “Hedhi”, “Maumivu” au “Hisia”.
  5. Chagua chaguo linaloelezea vizuri zaidi tukio au dalili yako.
  6. Rudia hatua hizi kwa kategoria zote unazotaka kufuatilia.
  7. Gusa “Hifadhi” ili kuhifadhi ulichofuatilia.

 


Kwa maswali mengine yoyote, vinjari orodha yetu ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara.
Unaweza pia kupata msaada kwenye video zetu za maelekezo

Was this article helpful?
0 out of 0 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk