Katika hali ya Clue Ufuatiliaji, unaweza kufuatilia mambo unayopitia yanayojirudia kwa mzunguko bila kuhitaji kufuatilia hedhi ili kuanza mzunguko mpya. Ili kuanza au kuweka alama ya mwanzo wa mzunguko mpya katika hali ya Clue Ufuatiliaji, una njia mbili:
- Kwenye mwonekano wa mzunguko, chagua siku na uguse aikoni ya kuanza ili kuanza mzunguko mpya.
- Nenda kwenye “Fuatilia”, chagua siku kwenye kalenda, chagua “Mwanzo wa mzunguko wa hedhi” kwenye orodha ya ufuatiliaji, kisha uguse “Hifadhi”.
------
Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii:
Instagram, TikTok na LinkedIn