Ninawezaje kuweka kikumbusho?

 

Unaweza kuweka na kubadilisha vikumbusho vyako vyote kwenye Menyu zaidi ya programu ya Clue.

Ili kuweka kikumbusho, fuata hatua hizi:

  1. Fungua programu ya Clue.
  2. Nenda kwenye Menyu zaidi, kwa kugusa alama ya “=” iliyo upande wa juu kulia kwenye Mwonekano wa Mzunguko.
  3. Gusa “Vikumbusho”.
  4. Gusa kikumbusho unachotaka kuweka.
  5. Washa kikumbusho.
  6. Gusa ikoni za penseli ili kubadilisha ratiba, muda au ujumbe wa kikumbusho. Chini ya mipangilio utaona mwonekano wa jinsi kikumbusho kitakavyoonekana kwenye kifaa chako.
  7. Sasa hakikisha kuwa umeruhusu arifa kutoka Clue katika mipangilio ya kifaa chako.
  8. Baada ya hapo, utapokea kikumbusho chako kwa wakati ulioweka.

Ikiwa hutaki tena kupokea kikumbusho, kizime tu kwenye Menyu zaidi > “Vikumbusho”.

 

------

Hujapata kile ulichokuwa ukitafuta? Angalia makala zifuatazo kwa maelezo zaidi kuhusu mada:

Ni vikumbusho gani vinavyopatikana katika programu ya Clue?
Je, ninaweza kutengeneza kikumbusho changu mwenyewe?
Sipokei vikumbusho vyangu. Ninaweza kufanya nini?

------

Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii: 
Instagram, TikTok na LinkedIn

Was this article helpful?
0 out of 1 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk