Ni uamuzi wako kama ungependa kuonana na mtaalamu wa afya kabla ya kutumia Clue Kutafuta Ujauzito. Kwa ujumla, ikiwa unafikiria kujaribu kupata ujauzito, inashauriwa kupanga miadi na daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake au wa uzazi kwa ajili ya ushauri kabla ya kupata ujauzito. Ukiamua kutokwenda kupata ushauri huo, pia ni sawa.
Ikiwa umekuwa ukijaribu kupata ujauzito kwa muda fulani, au una umri wa miaka 35 au zaidi, unashauriwa kuonana na mtaalamu wa afya huku ukiendelea kutumia Clue Kutafuta Ujauzito. Hii inaweza kukusaidia kutumia vizuri zaidi muda unaotumia kujaribu kupata ujauzito bila uingiliaji wa kitabibu.
Inashauriwa kuonana na mtaalamu wa afya katika hali zifuatazo:
- Ikiwa una umri wa chini ya miaka 35 na umekuwa ukijaribu kupata ujauzito kwa zaidi ya miezi 12.
- Ikiwa una umri wa kati ya miaka 35 na 39 na umekuwa ukijaribu kupata ujauzito kwa zaidi ya miezi 6.
- Ikiwa una umri wa zaidi ya miaka 40.
- Ikiwa una tatizo la afya ya uzazi kama vile endometriosis au uvimbe kwenye kizazi, au ikiwa mwenzi wako ana tatizo la kiafya linaloathiri korodani au amewahi kupata jeraha kwenye korodani.
------
Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii:
Instagram, TikTok na LinkedIn