Unapotumia hali ya Clue Kutafuta Ujauzito, utaona rangi mbalimbali katika Mwonekano wa mzunguko. Rangi hizo pia zinaonekana katika Mwonekano wa kalenda. Kila rangi inawakilisha hatua tofauti ya mzunguko wako na inaonyesha jinsi hatua hiyo inavyohusiana na uwezekano wa kupata ujauzito.
Hii ndiyo maana ya kila rangi:
- Nyekundu: Siku zako za hedhi.
- Kijivu: Siku ambazo uwezekano wa kupata ujauzito ni mdogo zaidi.
-
Bluu: Siku zako za rutuba kulingana na makadirio.
- Bluu hafifu: Siku zenye alama ya “Wakati mzuri”, ambapo uwezekano wa kupata ujauzito ni mkubwa zaidi.
- Bluu iliyokolea: Siku zenye alama ya “Wakati mwafaka”, ambapo uwezekano wa kupata ujauzito ni mkubwa kuliko siku nyingine zote.
- Nukta ya bluu hafifu ndani ya dirisha la uzazi: Siku ya uwezekano wa kuachilia yai.
Jifunze hapa unachoweza kufanya katika kila hatua ya mzunguko wako ili kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito.
------
Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii:
Instagram, TikTok na LinkedIn