Ninawezaje kutumia punguzo langu?

Ili kutumia punguzo lako, nakili na ubandike URL iliyo hapa chini kwenye kivinjari chako, ukiongeza msimbo wako mwishoni:

https://new.helloclue.com/checkout?discount_code= + {msimbo wako wa punguzo}

Kwa mfano, ikiwa una msimbo unaoitwa DISCOUNT50 (huu ni mfano tu na haufanyi kazi), URL itakuwa:

https://new.helloclue.com/checkout?discount_code=DISCOUNT50

Ukifungua ukurasa huu, unaweza kuingia au kufungua akaunti ya Clue ili kutumia punguzo lako. 

Ikiwa tayari una akaunti ya Clue, fuata maelekezo haya:

  1. Nenda kwenye URL ambayo msimbo wako umeongezwa.
  2. Gusa “Nina akaunti ya Clue”.
  3. Ingia kwenye akaunti yako ya Clue.
  4. Baada ya kuingia, msimbo wako wa punguzo utatumika kiotomatiki. 
  5. Weka taarifa zilizosalia za malipo na uanze usajili wako.
  6. Umemaliza! Sasa uko tayari kuanza kufuatilia kwenye programu yako ukiwa na manufaa yote ya Clue Plus.

Ikiwa huna akaunti ya Clue, fuata maelekezo haya:

  1. Nenda kwenye URL ambayo msimbo wako umeongezwa.
  2. Gusa “Mimi ni mgeni kwenye Clue”.
  3. Fuata maelekezo na uweke taarifa zako ili kufungua akaunti ya Clue.
  4. Baada ya kufungua akaunti yako, msimbo wako wa punguzo utatumika kiotomatiki. 
  5. Weka taarifa zilizosalia za malipo na uanze usajili wako.
  6. Umemaliza! Sasa uko tayari kuanza kufuatilia ukiwa na manufaa yote ya Clue Plus.
  7. Ikiwa bado hujafanya hivyo, pakua programu ya Clue kutoka Apple App Store au Google Play Store kisha uingie.

Kumbuka kuwa misimbo ya punguzo ya Clue Plus inaweza kutumika kupitia tovuti pekee, si kupitia programu. Bado utatumia programu ya Clue kufuatilia, lakini tumia tovuti ili kutumia punguzo lako. 

------

Hujapata kile ulichokuwa ukitafuta? Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii, angalia makala zifuatazo:

Kuna tofauti gani kati ya vocha ya Clue Plus na msimbo wa punguzo wa Clue Plus?
Msimbo wangu wa punguzo una muda gani wa matumizi?

------

Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii: 
Instagram, TikTok na LinkedIn

Was this article helpful?
0 out of 0 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk