Ikiwa una tatizo la kufikia Clue Plus baada ya kujisajili, fuata hatua zilizo hapa chini kulingana na kifaa chako.
ANDROID
- Angalia ikiwa una akaunti zaidi ya moja ya Gmail kwenye kifaa chako. Fungua Mipangilio > gusa sehemu ya “Akaunti” > tafuta taarifa za akaunti yako ya Gmail.
- Ikiwa una akaunti zaidi ya moja, fungua Google Play Store na uangalie ni akaunti gani unayotumia kuingia humo.
- Sasa hakikisha kuwa umeingia kwenye Google Play Store kwa kutumia akaunti ileile uliyotumia kufungua akaunti yako ya Clue na kununua usajili wako.
- Sasa unapaswa kuwa na ufikiaji wa Clue Plus katika programu yako ya Clue.
Ikiwa bado una tatizo, tafadhali wasiliana na timu yetu ya Usaidizi na ututumie kitambulisho cha muamala wa Clue Plus ili tuweze kuchunguza tatizo hilo zaidi. Utakipata katika barua pepe ya uthibitisho wa ununuzi kutoka Play Store, au katika sehemu ya “Shughuli nyingine za ununuzi” kwenye payments.google.com. Ni msimbo unaoanza na herufi “GPA”. Unaweza kuunakili na kuubandika katika ujumbe wako kwetu.
Pia, hakikisha kuwa unawasiliana nasi kwa kutumia anwani ileile ya barua pepe unayotumia katika Clue. Unaweza kuiona kwa kufungua menyu ya Clue (alama ya = katika kona ya juu kulia) na kuangalia sehemu ya juu ya ukurasa.
iOS
- Fungua programu ya Clue.
- Gusa Menyu zaidi katika kona ya juu kulia, kisha uguse bango la Clue Plus.
- Sasa utakuwa kwenye ukurasa wa kununua usajili.
- Sogeza chini na uguse “Rejesha Ununuzi”.
- Hatua hii itakagua upya ununuzi wako wote kupitia App Store na kurejesha taarifa sahihi za ununuzi katika programu ya Clue.
Ikiwa bado una tatizo, tafadhali wasiliana na timu yetu ya Usaidizi na ututumie risiti ya ununuzi wa usajili wako ili tuweze kuchunguza tatizo hilo zaidi. Risiti hiyo inapaswa kuwa na taarifa kama vile tarehe ya ununuzi, kiasi ulicholipa na sarafu uliyotumia, pamoja na kitambulisho cha agizo kinachohusishwa na usajili wako. Unaweza kunakili kitambulisho cha agizo na kukibandika katika ujumbe wako kwetu.
Ikiwa huwezi kupata kitambulisho cha agizo kinachohusishwa na usajili wako, fuata hatua hizi:
- Fungua Mipangilio kwenye kifaa chako.
- Gusa jina lako, kisha uguse “Media na Ununuzi”.
- Gusa “Angalia Akaunti”. Huenda ukaombwa kuingia katika akaunti yako.
- Gusa “Historia ya Ununuzi”.
- Sasa historia yako ya ununuzi itaonekana. Ikiwa huoni Clue Plus kwenye orodha, gusa “Siku 90 Zilizopita” na uchague kipindi tofauti.
- Chini ya ununuzi wako wa Clue, unaweza kupata kitambulisho cha agizo la Clue Plus (msururu wa herufi kubwa na nambari) upande wa kulia wa skrini. Unaweza kuinakili na kuibandika kwenye ujumbe wako kwetu.
Pia, hakikisha kuwa unawasiliana nasi kwa kutumia anwani ileile ya barua pepe unayotumia katika Clue. Unaweza kuiona kwa kufungua menyu ya Clue (alama ya = katika kona ya juu kulia) na kuangalia sehemu ya juu ya ukurasa.
------
Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii:
Instagram, TikTok na LinkedIn