Ikiwa umekuwa ukifuatilia data katika programu unayotumia sasa kwa muda, tunaelewa kwamba unaweza kusita kubadilisha programu ya kufuatilia hedhi. Lakini Clue imeundwa ili ikupe makadirio sahihi ya mzunguko wako hata tangu mwanzo.
Ni rahisi sana kufuatilia data za hedhi za zamani kwa kutumia kipengele chetu cha ufuatiliaji wa haraka. Andika tu tarehe za hedhi zako 3 zilizopita (au zaidi ikiwa unazo, ni bora zaidi) kutoka kwenye programu yako ya zamani, kisha fuata hatua zilizo hap ili kuzirekodi kwenye Clue.
Algoriti ya Clue inahitaji mizunguko 3 ya awali pekee ili kukokotoa kwa usahihi makadirio yake ya msingi. Makadirio hayo yanajumuisha tarehe za hedhi yako, dirisha la uzazi na siku ya ovulesheni. Tafadhali kumbuka kwamba ikiwa mizunguko yako si ya kawaida, algoriti inaweza kuhitaji data zaidi za mzunguko kabla ya kuwa sahihi zaidi.
Kwa dalili za mzunguko, kama PMS na maumivu ya hedhi, anza kuzifuatilia mara kwa mara kwenye Clue, na makadirio yataanza kupatikana hivi karibuni. Unaweza pia kuongeza data za mizunguko ya zamani mwenyewe kwa kurudi kwenye Mwonekano wa Kalenda wa Clue > Kugusa mara mbili tarehe unayotaka kuongeza data > Kufuatilia dalili zako > Kugusa “Hifadhi”.