Jinsi Clue inavyoshughulikia faragha ya taarifa

Faragha ya taarifa ni moja ya misingi ya maadili ya Clue. Tunajua kuwa ni muhimu kutoa programu ya kufuatilia afya iliyo salama, inayolinda faragha yako, na unayoweza kuamini. Daima tutajitolea kulinda faragha ya taarifa zako za afya na kuwa wazi kuhusu jinsi tunavyoshughulikia taarifa. 

Haya ndiyo mambo muhimu zaidi ya kujua:

  • Daima tutalinda taarifa zako, na tuko tayari kutetea ahadi hiyo kwa hali yoyote ile.
  • Clue haijawahi na haitawahi kushiriki taarifa binafsi za afya za mwanachama yeyote na mitandao ya matangazo.
  • Haijalishi uko wapi duniani, ukitumia Clue, taarifa zako zinalindwa na sheria kali zaidi za Ujerumani na Ulaya kuhusu faragha ya taarifa (GDPR).
  • Ikiwa mamlaka yoyote itadai kupata taarifa zako kupitia amri ya mahakama, hatutatii ombi hilo.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu ahadi yetu ya kulinda faragha ya taarifa hapa (kwa Kiingereza). Pia tunakuhimiza usome Sera ya faragha, ambapo tunaeleza kwa lugha rahisi na wazi jinsi Clue inavyoshughulikia uchakataji wa taarifa.

Pia tunaamini unapaswa kuwa na udhibiti mkubwa zaidi wa aina ya taarifa unazochagua kushiriki. Programu ya Clue inakupa uhuru huo kupitia mipangilio ya faragha yenye udhibiti wa kina, iliyo wazi, rahisi kutumia na inayoweza kubadilishwa kulingana na mapendeleo yako. 

Unapofungua akaunti yako ya Clue kwa mara ya kwanza, utaombwa kuchagua mapendeleo yako ya faragha na utapewa maelezo ya kina yatakayokusaidia kufanya uamuzi. Baada ya kuanza kutumia programu, unaweza kubadilisha mipangilio yako ya faragha wakati wowote. Kwa maelezo zaidi, angalia hapa (kwa Kiingereza).

Was this article helpful?
0 out of 0 found this helpful
Have more questions? Submit a request
Powered by Zendesk