Programu ya Clue inaweza kutumiwa na watu wawili kwenye kifaa kimoja. Kila mtu atahitaji kuwa na akaunti yake ya Clue.
Ili kubadilisha kati ya akaunti, fuata hatua hizi:
- Kwanza hakikisha kwamba watu wote wawili wamethibitisha anwani za barua pepe zilizounganishwa na akaunti zao za Clue.
- Fungua programu ya Clue.
- Toka kwenye akaunti ya mtu wa kwanza. Ili kufanya hivyo, nenda kwenye Menyu zaidi (alama ya "=" iliyo kwenye kona ya juu kulia ya Mwonekano wa Mzunguko wako) > Wasifu wako > "Toka".
- Funga programu.
- Fungua programu tena > Gusa "Nina akaunti" > Ingia kwenye akaunti ya mtu wa pili.
- Ili kuingia tena kwenye akaunti ya mtu wa kwanza, rudia hatua ya 3 hadi 5.
------
Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii:
Instagram, TikTok na LinkedIn