Ili kutumia vocha yako, nenda kwenye helloclue.com. Huko unaweza kuingia kwenye akaunti yako ya Clue au kufungua akaunti mpya ili kutumia vocha yako.
Ikiwa tayari una akaunti ya Clue, fuata maelekezo haya:
- Nenda kwenye https://helloclue.com/redeem.
- Weka msimbo wa vocha yako kisha uguse “Tumia”.
- Ingia kwenye akaunti yako ya Clue.
- Vocha yako imetumika! Sasa unaweza kufurahia manufaa yote ya Clue Plus bila kulipia.
Ikiwa huna akaunti ya Clue, fuata maelekezo haya:
- Nenda kwenye https://helloclue.com/redeem
- Weka msimbo wa vocha yako kisha uguse “Tumia”.
- Chagua “Jisajili sasa” chini ya chaguo za kuingia.
- Weka taarifa zako ili kufungua akaunti ya Clue.
- Vocha yako imetumika na usajili wako wa Clue Plus umeanza.
- Ili kuanza kufurahia manufaa ya Clue Plus, pakua programu ya Clue kwenye simu yako kwa kugusa kitufe cha App Store au Google Play Store.
Kumbuka kuwa vocha za Clue zinaweza kutumika kupitia tovuti pekee, si kupitia programu.
------
Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii:
Instagram, TikTok na LinkedIn