Huenda ukakumbana na matatizo ya kufuta akaunti yako ikiwa ulifungua akaunti ya Clue ukitumia maelezo yako ya kuingia ya Apple, Google au Facebook. Hii ni kwa sababu hukuunda nenosiri lako maalum ulipofungua akaunti yako ya Clue. Unahitaji kuwa na nenosiri ili kufuta akaunti yako.
Ili kuunda nenosiri la Clue sasa, fuata hatua hizi:
- Fungua programu ya Clue.
- Nenda kwenye Menyu zaidi, kwa kugusa alama ya “=” iliyo upande wa juu kulia kwenye Mwonekano wa Mzunguko.
- Gusa 'Usaidizi’.
- Gusa 'Maswali kuhusu akaunti’.
- Gusa 'Ninawezaje kufuta akaunti yangu ya Clue?”
- Gusa 'Nimesahau nenosiri langu’.
- Weka anwani ya barua pepe iliyounganishwa na akaunti yako ya Clue, kisha gusa "Tuma".
- Fungua barua pepe ya kubadilisha nenosiri uliyotumiwa hivi karibuni. Kumbuka kufanya hivi kwenye kifaa ambacho umepakua programu ya Clue.
- Gusa "Badilisha nenosiri lako".
- Chagua nenosiri jipya na gusa "Wasilisha".
- Sasa fungua tena programu ya Clue.
- Fuata hatua ya 2 hadi 5 zilizo hapo juu.
- Weka nenosiri lako na uguse “Futa akaunti”.
Ikiwa bado unakumbana na matatizo ya kufuta akaunti yako, wasiliana nasi kupitia fomu yetu ya mawasiliano.
------
Ungependa kujua zaidi kuhusu Clue? Tufuate kwenye mitandao ya kijamii:
Instagram, TikTok na LinkedIn